MAHITAJI NA VIPIMO
i. Siagi - Kikombe 1
ii. Sukari - Kikombe 1
iii. Unga - Vikombe 2
iv. Maziwa - 1/2 (nusu) Kikombe
v. Mayai - 4
vi. Baking Powder - 1 Kijiko cha supu
vii. Arki rose - kidogo
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA KEKI YA MAZIWA
A)JIKO LA OVEN
1. Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
7. Ipike (Bake ) mpaka iwive.
8. Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.
B)JIKO LA MKAA
washa jiko lako la mkaa.
2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6. Chukua sufuria umimine MCHANGANYIKO WAKO kisha uweke jikoni.
7. Weka sufuria ndani ya jiko na upike kwa muda wa dakika 30 hadi 40.
Hakikisha unathibitisha kuwa keki imeiva kwa kutumia kijiti kinachopenya ambacho kikitolewa kinapaswa kuwa kisafi.
8. Baada ya keki kuiva, toa kwenye jiko na iache ipoe kwa muda kabla ya kuitoa kwenye sufuria.
9. Unaweza kuiboresha kwa kuongeza glasi ya sukari juu ya keki au kuitumikia kama ilivyo, kulingana na mapendekezo yako.
Furahia keki yako ya nyumbani pamoja na familia yako au marafiki
Comments
Post a Comment